Latest Post
Showing posts with label events. Show all posts
Showing posts with label events. Show all posts

Upande Usiotakiwa Ujulikane Katika Historia ya Mapinduzi ya Zanzibar

Written By mahamoud on Thursday, 26 December 2013 | 11:36





Mohamed Omari Mkwawa (Tindo) mwanamapinduzi aliyesahauliwa,  mwamasishaji, mpelelezi, mtekelezaji mipango ya upigaji kura Zanzibar 1963, mwanamapinduzi Zanzibar 1964,  askari wa msituni wa Afro Shirazi Party, mvushaji askari mamluki wa Kimakonde na makabila mengineo kwenda Zanzibar kupiga kura na kushiriki katika mapinduzi akiwa amekishika kitabu Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru!

Mmoja wa washirika wa Mohamed Omari Mkwawa alikuwa Victor Mkello.

Photo

Kassim Hanga ni huyo aliyekaa chini ya jukwaa kavaa miwani. Aliyevaa sare ya polisi ni Hamza Aziz kushotoni kwake ni Andrew Shija aliyevaa pama. Aliyekaa mbele ya Kassim Hanga ni Omari Londo. Nyerere ndiye huyo katika ulingo akihutubia.  Hapo ni Mnazi Moja. Baada ya mkutano huu Hanga alirejeshwa Zanzibar na huko akauawa mwaka 1967 au 1968

Utangulizi
Kwa kipindi kirefu historia ya mapinduzi ya Zanzibarilikuwa ni ile historia rasmi ambayo imeathiri historia nyingi Afrika. Viongozi wa Afrika wanapenda ile historia itakayowakweza na kuwaonyesha wao katika mwanga wa kupendeza. Vinginevyo historia hiyo haitakiwi. Wazalendo wenyewe hawakuwa na hamu ya kuandika historia hii na watu wa nje walioandika historia ya mapinduzi ya Zanzibar hawakupata kuifanyia haki historia ya Zanzibar labda kwa ugeni wao na kwa kuyaamini maelezo yaliyokuwa “wazi” kwa wakati ule, mfano mkubwa ukiwa ni kule kuamini kuwa mapinduzi ya Zanzibar yalipangwa na makomredi wa Umma Party.

Hapajakuwapo udanganyifu mkubwa katika uandishi na utafiti kama huu. Dkt Ghassany amekiweka chano uwanjani bila kawa. Akizungumza na Abdushakur Aboud wa Sauti ya Amerika Dkt Ghassany amesema kuwa historia ya Zanzibar ni historia ya kujijuwa maisha yake akiwa mjukuu wa babu wa mababu Muomani na mabibi wa Kimanyema na Kimwera– mchanganyiko wa damu ya Kiarabu na Kiafrika. Hii kwa hakika ndiyo historia ya wananchi wa Zanzibar. Ni tabu sana kumpata huyo Muarabu Zanzibar kila umuonae Muarabu basi ana mjomba na shangazi Mwafrika. Maadui wa Zanzibar wakiweka mkazo katika ubaguzi wa rangi na kuwafitinisha Wazanzibari. Ukweli huu ndiyo chanzo cha matatizo yote yaliyoikumba Zanzibartoka vyama vya siasa vilipoanza katika miaka 1950 na matatizo yaliyosababisha mauaji ya mwisho yakiwa mwaka 2001.

Mohamed Omari Mkwawa
Mwaka 1995 wakati wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vyingi Tanzania nilibahatika kufuatana na mgombea urais wa CUF Prof. Ibrahim Haruna Lipumba katika kampeni za uchaguzi katika mikoa ya Kilimanjaro na Tanga. Prof. Lipumba alifanya mkutano mkubwa sana Tangamano kiasi cha kuishtua CCM. Baada ya mkutano ule Prof. Lipumba na ujumbe wake walialikwa nyumbani kwa mama mmoja akijulikana kama Mama Ummie (sasa ni marehemu) ambako walifanyiwa dhifa kubwa. Kote tukipita mitaa ya Tanga msafara wetu ulikuwa ukishangiliwa kwa nguvu sana. CUF ilikuwa imeingia Tanga kwa kishindo kikubwa.

Mimi kazi yangu ilikuwa kuangalia niliyokuwanayaona na kupiga picha. Kwa hakika nilikuwa nikishuhudia historia ikijiandika. Historia ambayo ilikuwa imeshahibiana sana na ile ya wakati wa kudai uhuru wa Tanganyikakatika miaka 1950. Lakini ninalotaka kusema si hili bali ni picha ambayo niliipiga ndani ya nyumba ya Mama Ummie. Picha hii ilikuwa inamuonyesha mzee mmoja wa makamo aliyevaa fulana ya CUF mbele ikiwa na picha ya Prof. Lipumba. Mzee huyu alikuwa amekaa nyuma ya Prof. Lipumba. Kwa wakati ule picha hii haikuwa na maana yoyote kwangu na hata nilipokuwa naitazama mara kwa mara sura yake si iliyokuwa inanivutia bali ile fulana ya CUF aliyovaa ambayo ilikuwa na picha ya rafiki yangu Prof. Lipumba.

Mungu ana mipango yake. Mihangaiko ya kutafuta riziki yakanihamishia Tanga na nikawa karibu sana na baadhi ya viongozi wa  CUF na wanachama wake. Sasa hapa ndipo nilipokujakuonana uso kwa uso na mzee yule kwenye picha yangu niliyoipiga hata kwa wakati ule ilikuwa miaka mingi iliyopita. Jina la huyu mzee wangu ni Mohamed Omar Mkwawa.  Ilikuwa katika barza yetu ya kawaida  ya kunywa kahawa na kula pweza huku tukijadili historia ya Tanzaniaambako siku moja Mzee Mkwawa alinambia, “Mohamed nataka nikuambie kitu. Unajua mimi nimehusika sana katika mapinduzi ya Zanzibar?”

Nilimuangalia Mzee Mkwawa kwa makini. Fikra yangu ya utafiti na uandishi ishashtuka haipo tena usingizini. Mzee Mkwawa aliendelea, “Mimi ndiye niliyekuwa nikiwavusha Wamakonde kutoka Kipumbwi kwenda Zanzibarkuipigia kura ASP na wakati wa mapinduzi mie ndiye niliyewavusha Wamakonde kwenda kuipindua serikali ya Jamshid.” Sasa moyo wangu ukaanza kudunda kwa nguvu. Naisemesha nafsi yangu, “Huyu mzee anajua uzito wa maneno haya?” Tuishie hapa. Kuanzia siku ile nikawa sasa namtazama Mzee Mkwawa kwa jicho jingine na heshima yangu kwake ikawa imepanda maradufu. Nilikuwa nimeshatambua kuwa Mzee Mohamed Omari Mkwawa alikuwa mmoja wa wanahistoria waliosahaulika katika historia ya Tanganyika na Zanzibar. Juu ya hayo nilishangazwa na kitu kimoja. Iweje leo huyu mwanamapinduzi wa ASP ambae Abeid Amani Karume alimpa jina la “Tindo” kwa ujasiri wake amekuwa mstari wa mbele CUF chama ambacho kinanasibishwa na Hizbu hasimu mkubwa wa ASP?

Dr Harith Ghassany
Nilikutana na Dr Harith Ghassany mwaka 1999 nyumbani kwake Maskati, Oman. Naikumbuka siku ile kama jana vile. Kanipeleka kwake mwenyeji wangu Farouk Abdulla lakini kabla ya kunipeleka nilikuwa nimeshalisikia jina lake mara nyingi sana pale Maskati kila nikikutana na jamaa wenye asili ya Tanzania jina lake litaibuka. Katika fikra yangu ikanijia kuwa Dkt Ghassany atakuwa ni mtu mzima. Sielewe kwa nini nilipata picha hii. Tulipopiga hodi na akatokea Dkt Ghassany kuja kutufungulia mlango nikapata mshangao mkubwa.

Aliyekuwa mbele yangu alikuwa ni kijana mdogo sana tofauti na nilivyodhani. Kwa njia ya utani hata kabla sijatoa salamu. Nikamgeukia Farouk nikasema, ”Ah! Dkt Ghassany, Dkt Ghassany, Dkt mwenyewe ndiye huyu?” Mila na tamaduni za watu wa pwani wakikutana hazipishani. Maskhara ni dalili ya mapenzi. Dkt Ghassany pale pale alipokea yale maskhara na akajibu, ”Bwana  wangu we wanakutisha bure kwani we ulidhani litakuwa jitu kubwa?” Urafiki na udugu wetu umedumu hadi leo na ndipo katika mazungumzo aliponifahamisha kuwa anataka kuandika historia ya kweli ya mapinduzi ya Zanzibar. Hapo ndipo nilipomjuvya kuhusu Mzee Mkwawa na nikamuomba aje Tanga amuhoji.

Kitu kimoja mashuhuri kwa mashujaa wa harakati za siasa katika Tanzania ni kuwa takriban wote wana hali ngumu sana za maisha. Sikujua vyema hali ya Mzee Mkwawa hadi nilipofika nyumbani kwake na Dkt Ghassany. Utu uzima na udhaifu wa maisha ulikuwa umempiga barabara. Nilimjulisha Dkt Ghassany kwa Mzee Mkwawa na kuwaacha waendelee na maongezi yao. Niliporudi mchana kumchukua Dkt Ghassany rafiki yangu alinambia nimuache nije jioni kumfuata. Niliporudi jioni nilimkuta Dkt Ghassany amechoka na uso umesawijika. Tukiwa ndani ya  gari yangu tunaondoka nikamuuliza kulikoni. Dkt Ghassany akanambia maneno ambayo hadi leo yamebaki kichwani mwangu, ”Mohamed ufunguo wa kitabu changu anao Mzee Mkwakwa na kama nisingeonana nae utafiti wangu wote wa kabla ungelikuwa hauna maana yoyote.”

Dkt Ghassany alikuwa amechukuliwa na Mzee Mkwawa katika safari ya zaidi ya nusu karne. Mzee Mkwawa akimshika mkono kwanza kumpeleka Pemba ambako akiwa kijana wa kiasi cha miaka 25 akifanya kazi ya uashi. Huo ndio ulikuwa wakati wa siasa za ASP na Hizbu zimepamba moto. Mzee Mkwawa alikuwa mmoja wa wachezaji wa ngoma ile hata kama alikuwa anatoka Tanganyika. Dkt Harith akavushwa na kuletwa pwani ya Kipumbwi na Sakura ambako Mzee  Mkwawa alikuwa akisimamia kambi ya mafunzo iliyokuwa msituni ya wakata mkonge wengi wao wakiwa Wamakonde, kambi ambayo ilitoa askari waliotumika kuipindua serikali ya Mohamed Shamte 12 Aprili 1964.

Dkt Ghassany hakuwa amejitayarisha kwa haya. Alishangwazwa na uwezo wa kumbukumbu wa Mzee Mkwawa, akitaja majina na mahali na akirudia mazungumzo neno kwa neno kati yake na maofisa wa serikali ya Tanganyika kutoka vyombo vya usalama waliomtia katika operesheni maalum ya kuipindua Zanzibar kutoka Tanganyika. Majina ya Abdulla Kassim Hanga, Jumanne Abdallah, Ali Mwinyi Tambwe, Victor Mkello, Oscar Kambona na wengine yakawa yanadondoka moja baada ya lingine. Taarifa hizi ndizo zilizommaliza Dkt Ghassany na kumsawajisha uso.

Mimi binafsi nilipigwa na butwaa. Nilibaini kama alivyobaini Dkt Ghassany kuwa Mzee Mkwawa alikuwa hazina na tulikuwa tumevumbua mgodi wa dhahabu. Kazi yetu sasa ilikuwa kuchimba tu. Kumekuwa na uvumi kwa miaka mingi katika duru za wanasiasa wapya na wa zamani na katika wanafunzi wa historia ya Tanzania na Mapinduzi ya Zanzibar kuwa Ali Mwinyi Tambwe alihusika sana katika kupinduliwa kwa serikali ya Zanzibar lakini hakuna aliyejuwa ni kwa kiwango gani na alihusika vipi. Lakini zito ni kuwa yeye mwenyewe akiudhika sana mtu akimuuliza habari zile. Kwa nini ilikuwa hivyo? Kitabu cha Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru cha Dkt Ghassany kilikuja kutoa majibu. Hakuna binadamu apendae historia yake ihusishwe na mauaji na dhulma na kufutwa kwa nchi yake.

Kwa kipindi cha takriban miaka saba Dkt Ghassany alikuwa akija Tanga kwa mahojiano na Mzee Mkwawa na katika kipindi hicho Mzee Mkwawa alitupeleka Kipumbwi na Sakura na kutuonyesha sehemu zile ambazo walikuwa na kambi na wakifanya mazoezi ya kivita na matumizi ya silaha. Mkahawa ambao wale wakata mkonge walikuwa wakila chakula cha usiku kabla ya kuvushwa kwa vyombo vya bahari kwenda Unguja bado upo hadi leo ingawa kwa sasa kijumba kile hakitumiki tena kama mkawaha. Endapo itakuja siku serikali ya Zanzibar itataka kuhifadhi historia ya Mapinduzi ya Zanzibar bila shaka moja ya vitu vitakavyokuwa katika makumbusho ni picha ya hicho kibanda.

Victor Mkello
Kipumbwi haijabadilika iko kama vilevile iliyokuwa miaka ya 1960.  Kipumbwi imebaki vilevile kama kijiji cha uvuvi. Mzee Mkwawa alitupeleka hadi sehemu ambapo bahari imeingia katika kijiji lakini sehemu hiyo imefunikwa na mikoko mingi na vichaka. Tuliingia ndani na kuangalia mandhari ya pale mahali. Hakika pale palikuwa sehemu nzuri ya kujificha. Leo imekuwa sehemu hii ni maarufu kwa watu wa magendo.  Mzee Mkwawa alitueleza kuwa hapo ndipo walipojificha na ndipo walipopandia vyombo vyao kwa usiri mkubwa wakati wote wakiwa wamevaa nguo matambara na kofia za makuti kama wavuvi. Tanga ilikuwa kituo muhimu cha kufanikisha mapinduzi ya Zanzibar. Haikuwa bure kuwa Ali Mwinyi Tambwe, Jumanne Abdallah na Victor Mkello walikuwa hapo na wala haistaajabishi kwa Dkt Ghassany kutueleza kuwa vinara wa mapinduzi kwa upande wa bara, Mkello na wenzake, walisubiri taarifa za mapinduzi katika mkesha ndani ya ofisi ya TANU Tanga.

Napenda kukiri kuwa sikupata kushiriki kama msikilizaji wa mahojiano wakati wa utafiti wa Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru. Kazi yangu kubwa sana ilikuwa kufungua milango na kumwendesha daktari. Kwa ufupi kazi yangu ilikuwa kumwekea mwandishi mazingira mazuri ili kazi yake iwe nyepesi. Kwa hakika ilikuwa kazi ambayo na mimi vilevile nilisoma, kujifunza mengi na kupata faida kubwa. Katika haya nakumbuka sakata la kumtafuta Victor Mkello. Leo si wengi wanaomjua Victor Mkello au hata kupata kusikia jina lake likitajwa. Lakini kwa sisi tuliokuwa wadogo tukiwa shule katika miaka ya 1960 Mkello alikuwa hapungia katika magazeti ya Ngurumo na Mwafrika. Mzee Mkwawa ndiye aliyetusaidia kumtafuta alipo. Victor Mkello ndiyo aliyekuwa ”Amiri Jeshi Mkuu” wa lile jeshi la Wamakonde lililokuwa na makao yake makuu katika mashamba ya mkonge ya Sakura na Kipumbwi. Bila ya kupata kauli ya Mkello kitabu kisingeweza kuandikika.

Ilichukua muda kuweza kumpata. Kwanza tulikwenda Muheza ambako ndiko kwao. Huko tukaambiwa kuwa hakuwapo hapo bali kwa muda mrefu alikuwa Tanga. Mwishowe tulimkuta nyumbani kwake Nguvu Mali. Mkello alikuwa katika kitanda cha mauti. Kisukari kilikuwa kikimla kiwiliwili chake. Hakuwa anaweza kunyanyuka kitandani wala kukaa. Kwa hakika alikuwa anasikitisha. Huyu hakuwa Victor Mkello niliyekuwa namsoma katika magazeti wala yule ambae Mzee Mkwawa alikuwa akituelezea. Mtu mjanja aliepambana na Magiriki wamiliki wa mashamba ya mkonge akitetea haki za Waafrika katika miaka ya 1960. Huyu kwa kweli hakuwa yule Victor Mkello aliyekuwa akisaidiana na TANU na Mwalimu Julius Nyerere kupigania uhuru wa Tanganyika. Hiki mbele yetu kilikuwa kivuli chake. Hapakuwa na wasiwasi wowote Victor Mkello alikuwa akisubiri malaika wa mauti amtembelee na yeye hilo alikuwa akilijua fika.

Victor Mkello na Mzee Mkwawa wanamapinduzi waliofutwa katika historia walitazamana na wakasalimiana kama vile hakuwapata kujuana. Jicho la Mkello lilikwenda kwa Dkt Ghassany kisha likaangukia kwangu kisha likarudi kwa mwanamapinduzi mwenzake Mzee Mkwawa. Baada ya utambulisho uliofanywa na Mzee Mkwawa nilihisi woga na wasiwasi kwenye sura ya Victor Mkello. Hakuwa anaamini kuwa Dkt Ghassany katoka Maskati kwa ajili ya utafiti wa historia na hili lilijidhihirisha alipofunua kinywa kuzungumza. Victor Mkello alikuwa na hisia kuwa alifuatwa kukamatwa kwa vifo vya Waarabu vilivyotokea Zanzibar wakati wa mapinduzi ili apelekwe Mahakama ya Kimataifa. Baadae Dkt Ghassany alinifahamisha kuwa jinsi Waingereza walivyomueleza katika taarifa zao za siri ambazo yeye alizisoma London zimeafikiana kabisa na jinsi alivyomuona pale. Waingereza walimsifia Mkello kwa kusema kuwa alikuwa bingwa wa kuteleza kama samaki ndani ya maji.

Kufupisha maelezo. Ilichukua karibu miaka mitatu kwa Victor Mkello kukubali kuzungumza kuhusu mapinduzi ya Zanzibar. Dkt Ghassany akienda Maskati na kurudi Tanga na kila akienda kwa Victor Mkello, Mkello hakuwa tayari kueleza kile alichokijua kuhusu mapinduzi ya Zanzibar. Kila nilipokwenda na Dkt Ghassany kumuona Mkello hali yake ilikuwa inazidi kudidimia. Sasa alikuwa kakatwa mguu mmoja kwa ajili ya kisukari. Ilikuwa katika hali ile katika siku zake za mwisho ndipo siku moja alipomwambia Dkt Ghassany aje siku ya pili na yeye atazungumza na angependa azungumze mbele ya mkewe ili amkumbushe pale atakapokuwa kasahau kitu.

Hapa ndipo ilipo moja ya sehemu tamu kabisa ya kitabu hiki Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru. Victor Mkello Amiri Jeshi Mkuu wa Mamluki wa Kimakonde alizungumza. Mimi sikushiriki katika mazungumzo yale nilijiweka pembeni ili Mkello azungumze na Dkt Ghassany kwa utulivu. Nilikuwa nimeegesha gari yangu karibu ya msikiti jirani ya nyumba ya Mkello nikimsubiri daktari akamilishe upasuaje mgonjwa apate nafuu. Mwendo wa Dkt Ghassany wa kudunda alipokuwa ananijia pale nilipoegesha gari ulidhihirisha furaha yake.

Haukupita muda mrefu baada ya mazungumzo yale na Dkt Ghassany, Victor Mkello akaaga dunia kimya kimya. Hakuna mtu aliyejua kifo chake kama ilivyokuwa vifo vingi vya mashujaa waliopigania uhuru wa Tanganyika. Hakuna hata gazeti moja lililotoa taazia yake wala hotuba hazikusomwa kaburini kwake. Mkello aliondoka katika historia ya Tanzania kimya kama jinsi mamluki wake walivyokuwa wakiingia Zanzibar kimya kimya usiku mkuu  na kwa siri, mapanga yao makali ya kukata mkonge yakiwa chini ya nguo zao za ndani yakisubiri kuivamia Zanzibar na kuua watu wasio na hatia. Kazi hii kwao haikuhitaji mafunzo kwani  mafunzo walikuwanayo muda mrefu katika kazi yao ya kukata mkonge katika mashamba ya mkonge ya Tanga. Pigo moja lilitosha kuangusha chini jani zito la mkonge seuze kiungo cha binadamu.

Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuruni kitabu kilichoandikwa kwa staili ya pekee wahusika wenyewe wa matokeo katika mapinduzi kujitolea kueleza kile kilichotokea katika mapinduzi, kabla na baada yake. Kuanzia mipango ya kuangusha serikali ya Zanzibar hadi katika kuwaua wale waliokujakushukiwa kuwa ni maadui wa mapinduzi hadi kufikia hata kuweka wazi jinsi walivyoshiriki katika mengi ya kusikitisha kupelekea hata msomaji kujiuliza kwa nini hawa watu baada ya miaka yote hiyo kupita wameamua kueleza yote hayo. Vipi Abdallah Kassim Hanga, Othman Shariff, Mdungi Ussi, Jaha Ubwa, Abdulaziz Twala na wengineo walivyouliwa, nani alitoa amri ya mauaji, nani aliwauwa na katika mazingira gani. Kifo cha Karume mwenyewe kwa mtutu wa bunduki hakikuwekewa pazia na chanzo cha kuamuliwa kuwa auawe ni tofauti ya kilichozoeleka kuelezwa. Karume hakuuawa na ”wapinga mapinduzi” kama ilivyozoeleka kuelezwa katika historia rasmi.

Kwa kumaliza tusubiri mapitio ya kitabu hiki na ni wazi kuwa wasomaji watapata mengi ya kuelimisha na kuhuisha. Tunategemea wasomi wa somo la historia watakaopitia kitabu hiki watatufanyia hisani kubwa kwa kuwaleta katika picha wahusika wakuu wa mapinduzi – Mwalimu Julius Nyerere – fundi mkuu mwenye kishindo kikubwa lakini hakisikiki, mkono wake wa chuma hauonekani, uso wake nyuma ya pazia, Abdallah Kassim Hanga – kiongozi hasa na mpangaji wa mapinduzi, Victor Mkello – mtumishi wa Hanga na Nyerere  bila ya yeye mwenyewe kujua kati ya hao wawili nani aliyekuwa bingwa kumshinda mwenzake katika mchezo mchafu wa siasa ya kuiuwa Zanzibar na Wazanzibari na wengineo.

Lakini juu ya hayo yote mipango hii ilikuwa ni ya akina Nyerere, Hanga na Mkello pekee? Dkt Ghassany anaeleza nini kuhusu mkono wa Waingereza, Algeria, Misri, Wachina, Warusi, Marekani na Mayahudi? Nini kilichowasukuma hao wote katika mapinduzi ya Zanzibar? Nini kilimsukuma Nyerere, kuwapindua Waislam walioupigania Uhuru wa Tanganyika na baadae kuwapinduwa Waislam walioupigania Uhuru wa Zanzibar na kuendelea kuwadhibiti hata baada ya kuipindua Zanzibar? Nini kilichowasukuma Waingereza na Wamerekani kuachia mapinduzi yafanyike? Lakini kubwa zaidi kipi kilichowasukuma Wayahudi kuingia na kusaidia mapinduzi, ni ile chuki yaoya asili dhidi ya Waarabu au kulikuwa na jengine ambalo liliwatia khofu? Na kwanini kitabu kiitwe Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru: Zanzibarna Mapinduzi ya Afrabia? Kitabu kina majibu ya haya maswali mengine ambayo bado hayajaulizwa na chemchemu mpya za utafiti.

Dkt Ghassany anastahili pongezi kubwa sanakwa kuinusuru historia ya mapinduzi ya Zanzibarna kuwaamsha Wazanzibari na Watanganyika toka lepe zito la usingizi ili wajitambue na wamjue adui yao. Anastahiki pongezi kubwa zaidi si kwa kukiandika kitabu cha Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru bali kwa kutumia mrengo usiokuwa na mrengo. Huna pa kumuweka Dkt Ghassany na baada ya kumaliza kukisoma kitabu ukaridhika napo. Kamautafikiria kuwa kitabu ni cha CUF basi baada ya kusoma mpaka mwisho utavunjika moyo. Kama utamtumbukiza ndani ya CCM basi ataelea. La kama unataka upae nje ya masunduku na mapakacha basi utamuona katulia ndani ya uhuisho wa umoja wa Zanzibarna Tanganyika Mpya – Tanzania Mpya.

Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru ni ngoma nzito ambayo watu wameanza kuicheza hata mdundo haujaanza kupigwa! Tayari imeshaingia katika rikodi za Hansard za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tayari imeshasikika katika Sauti ya Marekani. Tayari daktari anafuatilia kwa karibu ukweli wa Maridhiano na kuwa kwa mara nyengine tena ukweli wake umeshaanza kupotoshwa na waroho na tayari historia mpya na kubwa zaidi hata kuliko ile ya Mapinduzi ya Zanzibar ya 1964 imeshaanza kuvurugwa.

Watengenezaji wa filamu Hollywoodwana mtindo wa kumaliza senema zao za matokeo ya kweli kwa kueleza katika maandishi yale yaliyowafika wahusika wa kisa kilichotengenezwa hiyo senema. Huonyesha majina na mwisho wa hao wahusika, kama wahai, wako wapi, wamekufa na kama wamekufa ni kwa kuuliwa au kwa amri ya Mungu nk. Katika Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru majina ya wahusika machache ambayo yametajwa katika makala haya yako kamahivi:

1.     Mohamed Omar Mkwawa:           Yu hai na anaishi Makorola Tanga
2.     Abeid Amani Karume:                            Ameuawa 1972
3.      Abdallah Kassim Hanga:             Ameuawa 1967/68
4.     Mustafa Songambele                      Yuhai anaishi Songea.
5.     Victor Mkello                                  Amekufa kifo cha kawaida
6.     Ali Mwinyi Tambwe                      Baada ya mapinduzi alikuja kuhusika katika mchakato wa kuunda muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Amekufa kifo cha kawaida.
7.     Jumanne Abdallah                         Alitumikia serikali kwa muda mrefu hadi alipofariki kifo cha kawaida
8.     Oscar Kambona                              Aligombana na Nyerere na akakimbia nchi mwaka 1967 na kwenda kuishi uhamishoni Uingereza
9.     Kuna vigogo kadhaa ambavyo viko hai na kwa sasa wameomba majina yaoyahifadhiwe.

17 Ramadhani 1431

28 August 2010

Photo

Ali Mwinyi Tambwe na Abeid Amani Karume



Abdalla Kassim Hanga

Kuwa Hanga ndiye aliyekuwa kinara wa Mapinduzi ya Zanzibar hili si jambo lenye utata tena. Ikiwa hivyo ndivyo Hanga hatoweza kuutua mzigo wa roho zilizopotea katika mapinduzi hayo. Ikiwa Hanga atalaumiwa kwa vifo vya maelfu ya Wazanzibari nani alaumiwe kwa umauti uliomfika Hanga tena kwa kuuliwa kishenzi kwani hapana neno zaidi ya hilo linaloweza kutosheleza kuelezea jinsi Hanga alivyouliwa. Kichekesho kikubwa ni kuwa wale waliopoteza roho kwa hiyo kutangulia mbele ya haki, yao yalikuwa yamekwisha. Lakini kwa wale wajane na mayatima waliobakia nyuma wakihangaika, kifo cha Hanga na wenzake katika wale waliofanikisha mapinduzi kuuliwa kwao kulikuwa muujuza wa aina yake, uchawi usioelezeka nani fundi wake. Ilikuwa vigumu kueleza. Ingeeleweka vyema endapo kisasi cha kuitoa roho ya Hanga kingetimizwa kutoka katika mikono ya maadui zake waliopinduliwa. Haikuwa hivyo.

Wale wajane na mayatima walililipiziwa kisasi na watu waliokuwa maadui wakubwa wa waume na baba zao waliopinduliwa. Vipi Hanga kiongozi mkuu wa mapinduzi aje kuwa adui wa mapinduzi yenyewe kiasi cha kuwa hukumu ya kumtosheleza haikuwa kifo tu bali kifo cha kishenzi. Fikra ya Hanga ilikuwaje alipokuwa peke yake ndani ya selo Ukonga Prison…usiku ukimpita bila ya hata lepe la usingizi akiwaza yanayomkabili. Nini kilikuwa kikipitika katika ubongo wake wakati wauaji wake walipomtoa katika selo yake na yeye akawakabili ilhali aikijua kuwa walikuwa wamekuja kuitoa roho yake. Fikra yake ilikwenda wapi? Ilikwenda kwa Sultan Jamshid bin Abdullah aliyempindua na kwa Masultani wengi waliopita ambao wameiaga dunia mikono yao ikiwa haina damu au kwa Abeid Amani Karume aliyeingia madarakani kwa mapanga ya Wamakonde kutoka Tanganyika, wakata mkonge kutoka Tanganyika wakifanya kazi mashamba ya Sakura na Kipumbwi? Fikra ya Hanga ilielekea wapi? Kwa Nyerere aliyemsaliti?

Hakika ni wazi hakutegemea mapinduzi aliyoyasisi yangemgeukia na kuwa sababu ya yeye kutolewa roho kwa kuuliwa kishenzi. Jambo la kusikitisha ni kuwa hadi pale alipokamatwa na kuwekwa jela Ukonga na kufikishwa mbele ya mkutano wa hadhara na kuadhiriwa na Julius Nyerere tayari alikuwa keshapoteza kila kitu achilia mbali dira ya mapinduzi aliyokusudia ingeongoza Zanzibar. Hanga hakuwa kamwe na uwezo wa kumfanya Karume lolote kwani Karume tayari alikuwa chini ya mbawa za Nyerere ngome ambayo Hanga asingeweza kuitikisa achalia mbali kuibomoa. Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar ilikuwa hirizi tosha ya kumkinga Karume.

Katika mkasa wa kuuliwa kwa Hanga ndipo msemaji mmoja akasema, “Maiti toka makaburini mwao walionyesha ujuzi wa kufanya miujiza na uchawi wao kwani laiti kifo cha Hanga kingesababishwa na wale waliopinduliwa kisasi chake kingekuwa cha kutisha. Ilibidi Hanga kwa miujiza ya maiti zile auliwe na wale wale aliowaweka madarakani watu ambao hapakuwepo na sababu ya wao kumuona adui. Halikudondoka chozi kwa kifo cha Hanga. Kila aliyepata mnong’ono wa kuuliwa kwake alikuwa kimya kama vile ile taarifa ile ya kifo haimuhusu.


10 February 2010
Nyuma ni pwani ya Kipumbwi ambako wakata mkonge kutoka mashamba ya mkonge ya Sakura walipokuwa wakingoja
usiku uingie ili wavunshwe na majahazi kwenda Zanzibar kupindua serikali

Mwandishi akifanya mahojiano ya televisheni  (TV Imaan) na aliyekuwa katibu wa kwanza wa
 Baraza la Mapinduzi  Zanzibar  Salim Rashid 
Aliyevaa shada la maua ni Mohamed Abdulrahman Babu, pembeni yake Ali Muhsin Barwan na mwisho
ni Mohamed Shamte 
Waliokaa kushoto ni Abdallah Kassim Hanga akifuatiwa na Abeid Amani Karume

MAPITIO YA KITABU SIMBA WA VITA KATIKA HISTORIA YA TANZANIA RASHIDI MFAUME KAWAWA

MAPITIO YA KITABU SIMBA WA VITA KATIKA HISTORIA YA TANZANIA RASHIDI MFAUME KAWAWA

Na Mohamed Said

Kwa mara ya kwanza Tanzania ilishuhudia kuandikwa kwa historia ya mmoja wa viongozi wakuu wake kupitia kitabu “Simba wa Vita Katika Historia ya Tanzania Rashidi Mfaume Kawawa” kilichoandikwa na Dk. John M. J. Magotti. Sidhani kama katika historia ya Tanzania kuna kumbukumbu ya kuandikwa kwa kitabu kinachohusu maisha ya kingozi yoyote achilia mbali kufanyika kwa sherehe ya kukizindua kitabu hicho Ikulu ikiongozwa na rais mwenyewe.  Kwa hakika sherehe ilifana sana na tukakisubiri kwa hamu kitabu madukani ili tupate kunufaika na kumbukumbu za Mzee Kawawa.

Msomaji anaweza kukisoma kitabu chote chenye kurasa 127 kwa muda wa saa moja akawa kakimaliza chote na atakapokiweka chini akawa hakubakia na chochote cha maana katika fikra yake. Kwa nini iwe msomaji asibaki na kumbukumbu yoyote ya kiongozi mkubwa kama Mzee Kawawa mtu aliyeshuhudia kwa macho yake mwenyewe harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika na si hivyo tu yeye mwenyewe ni mmoja wa wale waliopigania uhuru wa Tanganyika na kushika nyadhifa kubwa za uongozi chini ya Mwalimu Julius Nyerere. Kwa kawaida vitabu vya maisha ya viongozi hasa wapigania uhuru huwa vina mambo mengi sanaambayo kwa muda mrefu huwa siri, hayafahamiki hadi hapo kitabu kitakapoandikwa ama kwa mkono wake kiongozi mwenyewe au kuandikwa na muandishi. Mifano ipo mingi. Kitabu kama “Mahatma Gandhi” klichoandikwa na Robert Payne au “Long Walk to Freedom” alichoandika Nelson Mandela mwenyewe au “Seeds of Freedom” alichoandika Bildad Kaggia hakika unapomaliza kusoma vitabu hivi lazima urudi nyuma kufungua kurasa hapa na pale kuzisoma upya zile sehemu zinasosisimua.

Huwezi kupata haya katika kitabu cha Mzee Kawawa. Huwezi kuyapata haya kwa kuwa mwandishi hakuandika kitu. Hakuandika kitu si kama Mzee Kawawa hana historia ya kusisimua na kuwa hana mengi ambayo wengi hawayajui katika maisha yake, nadhani mwandishi hakuwezakuja na jipya labda kwa sababu hakufanya utafiti wa kutosha kuweza kuandika kitabu kinachomuhusu simba wa vita aneunguruma. Kuna msemo wa Kiswahili usemao “Aungurumapo simba mcheza ni nani?” Kwa hakika simba wa vita hakuunguruma kabisa katika kitabu hiki. Sijui lawama zielekezwe wapi.

Mimi simjui Mzee Rashidi Kawawa kwa kiwango cha kusema naweza kunyanyua kalamu na kufanya pitio la kitabu kilichoandikwa kuhusu yeye. Nathubutu kuandika kuhusu kitabu chake kutokana na kumjua kwangu mimi nikiwa kama mwandishi na mtafiti ambae katika kutafiti kwangu nimekutana na jina la Mzee Kawawa hapa na pale katika nyaraka zilizo katika hifadhi ya ukoo wa akina Sykes. Nitatumia uzoefu wangu huu kueleza yale niliyoyaona katika nyaraka hizi na ninayojua kuhusu Mzee Kawawa na kufanya tathmini kwa yale niliyoyasoma katika kitabu cha Magotti.

Miaka kama ishirini iliyopita nikiwa kijana mdogo nilipata hamu ya kuandika historia ya kudai uhuru wa Tanganyika. Sikuona mtu wa kumuendea isipokuwa Ally Sykes. Nilipomueleza kuwa nia yangu ni kuandika kitabu kuhusu marehemu kaka yake Abdulwahid Sykes (1924- 1968) Ally Sykes alinambia kuwa atanipa nyaraka zake zote nizipitie kisha ndiyo nakaenae chini kwa mahojiano ya ana kwa ana. Katika nyaraka alizonikabidhi ndani yake nilikuta barua ya mkono aliyoandika Rashid Kawawa mwaka 1952 kutoka Bukoba akimletea Ally Sykes aliekuwa Dar es Salaam. Barua hii ya Mzee Kawawa kwa Ally Sykes ilikuwa ikimfahamisha Ally Sykes hali ya siasa Kanda ya Ziwa. Hii barua hadi leo ipo katika nyaraka za akina Sykes. Nilipokaa na Ally Sykes kutaka maelezo ya barua ile aliyoandikiwa na Kawawa, Ally Sykes alinipa kisa hiki:

Mwaka 1951 nilichaguliwa kuwa katibu mkuu wa Tanganyika African Government Servants Association (TAGSA). Chama hiki kiliundwa mwaka wa 1927 kwa lengo la kuendeleza maelewano mazuri baina ya serikali ya Malkia na sisi watumishi Waafrika. Rashid Kawawa alikuwa mwana kamati. Mimi nilichaguliwa pamoja na Thomas Marealle kama rais wa TAGSA. Katiba ya TAGSA iliamuru uchaguzi wa kila mwaka, na mimin nilirudishwa madarakani kama katibu mara nne hadi Oktoba, 1954 nilipojiuzulu baada ya kuhamishwa kwenda Korogwe kamaadhabu kwa kuwa miongoni mwa wale wanachama 17 waliounda TANU. Watu kadhaa walishika urais. Stephen Mhando na Dr Wilbard Mwanjisi wote hao waliwahi kuchaguliwa kuwa marais wa TAGSA. Miongoni mwa wanachama watendaji wa TAGSA walikuwa Dr Michael Lugazia na Rashid Kawawa ambao alichaguliwa kuwa katibu baada ya mimi kujiuzulu. Kupitia TAGSA, Kawawa alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Tanganyika Federation of Labour (TFL).

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa ulipokuja kuzuru Tanganyika Agosti, 1951 kwa mara ya tatu, vyama vyote viwili, TAA na TAGSA, viliwakilisha malalamiko kwa ujumbe huo. TAGSA iliwakilisha malalamiko yake kuhusu ubaguzi katika utumishi serikalini kwa mujibu wa kupanga mishahara kufuatana na rangi ya ngozi. Mshahara wa Mwafrika ulikuwa wa chini zaidi kuliko ule aliokuwa akipokea Mzungu au Muasia kwa kazi hiyo hiyo. Kwa mfano Mwandishi wa hati mkato Mzungu alikuwa akipata mshahara mkubwa kuliko Mwafrika aliyekuwa na shahada au digrii kutoka chuo Kikuu cha Makerere. TAGSA vilevile tulilalamika kuhusu kuajiri makarani wa kutoka India na hali walikuwepo Waafrika kutoka Afrika ya Mashariki na Nyasaland ambao wangeweza kujaza nafasi hizo kwa urahisi.

Vyama vyetu hivi viwili TAA na TAGSA viliwakilisha malalamiko haya tukifahamu fika kwamba Uingereza ilikuwa ikiitawala Tanganyikachini ya vifungu nambari 76 na 77 vya Umoja wa Mataifa ambavyo viliwekwa ili kuendeleza maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ya nchi zilizokuwa chini ya udhamini. Kama mdhamini Uingereza ilitakiwa kuhimiza na kuheshimu haki za binadamu na uhuru wa kwa wote bila kubagua kwa misingi yajinsia, lugha au dini. Lakini Uingereza ilikuwa ikipuuza vifungu hivi bila aibu. TAGSA tuliwakilisha malalamiko haya ili Umoja wa Mataifa ujue matatizo halisi ya ukoloni nchini Tanganyika.

Mimi nikiwa katibu wa TAGSA nilifuatilia serikalini masuala yaliyoainishwa ndani ya malalamiko yetu. Suala lililokuwa likituhangaisha sanawakati ule ilikuwa uajiri wa Wahindi kutoka India, jambo ambalo niliieleza serikali halikuwa na faida, maadam kulikuwako na Waafrika ndani ya nchi ambao wangeweza kujaza nafasi zile. Jambo hili lilikuwa likisababisha manugíuniko makubwa miongoni mwa Waafrika. Hakuna majibu maridhawa yaliyopatikana kutoka kwa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa. Barua tulizoandika serikalini juu ya masuala hayo zilipuzwa na Chief Secretary, Bruce Hutt. Katika kufuatilia malalamiko haya, Niliandika barua moja kali sana na kwa mara ya kwanza bila kutafuna maneno niliuliza uhalali wa Waingereza kututawala Waafrika wa Tanganyika. Nillimwambia Katibu Mkuu kuwa kwa kuwa serikali imeshindwa kupata ufumbuzi kwa matatizo ya Waafrika, Uingereza lazima ijitoe Tanganyikana Umoja wa Mataifa utawale Tanganyika. Barua hiyo ilimkasirisha Katibu Mkuu na siku chache baadaye nilipokea barua kutoka serikalini iliyokuwa imejaa vitisho, dharau, stihizai na makemeo. Nikajibiwa kuwa hakuwa na suala la Umoja wa Mataifa kutekeleza utawala wa moja kwa moja Tanganyika.

Dkt Mwanjisi alikuwa amegusa suala nyeti sanakwa kuzungumzia matatizo ya ubaguzi wa rangi uliokuwa ukitukabili Waafrika wa . Kawawa, kama mjumbe wa kamati, akaniandikia barua akanitahadharisha nisichapishe ile hotuba ya Dkt Mwanjisi katika jarida la TAGSA bila idhini ya kamati ya utendaji. Kufuatia majibishano haya kati ya TAGSA na serikali, Dkt Mwanjisi kama alivyofanyiwa Dk Kyaruzi kabla yake, akahamishwa kutoka hospitali ya Sewa Haji mjini Dar es Salaamhadi Kingolwira Prison Hospitalkaribu na Morogoro. Kawawa na yeye akapewa uhamisho kwenda Bukoba na mimi nikapewa uhamisho kwenda Mtwara. Dk Mwanjisi na Kawawa walikubali uhamisho wao na wakaondoka Dar es Salaam. Mimi nilikataa uhamisho na nikabakia Dar es Salaam kupinga uhamisho wangu.

Alipokuwa Bukoba ndipo Kawawa akamwandikia Ally Sykes barua ile ya mwaka 1952 akimweleza hali ya siasa kamaalivyoikuta Kanda ya Ziwa. Huyu ndiye Kawawa niliyemjua mimi kupitia nyaraka na mahojiano na Ally Sykes. Kwa kweli inasikitisha kuwa Dk Magotti hakupata fursa ya kuziangalia nyaraka hizi muhimu sana katika siyo historia ya Kawawa bali katika historia ya kuundwa kwa TANU na kudai uhuru wa Tanganyika. Endapo angepata nafasi ya kuziona hizi nyaraka zingempelekea katika kuwajua wazalendo wengine waliotajwa mle ndani kama Dk. Kyaruzi, Dk. Wilbard Mwanjisi ambao Kawawa alikuwanao katika harakati za TAGSA. Katika majina hayo angeweza kudodosa mengi kutoka kwa Mzee Kawawa na hivyo kuandika yale ambayo hayafahamiki kwa wengi. Hii imgekifanya kitabu kiwe cha maana.

Mathalan Kawawa angeeleza mtafaruku kati ya Mwalimu Nyerere na Dk. Mwanjisi nini chanzo chake na nini ikajakuwa matokeo yake. Halikadhalika angempa fursa Mzee Kawawa kumuhadithia mchango wa Dk. Michael Lugazia katika kuasisi kwa TANU hasa kipindi kile cha 1953 wakati TAA ilipokuwa inatayarisha rasimu ya katiba ya TANU. Kwa ufupi ni kuwa Dk Lugazi alikuwa akijaribu kuamsha ari ya TAA Bukoba ari iliyokufa kutokana na kufungwa kwa kiongozi wa TAA Bukoba Ali Migeyo. Kisa cha Ali Migeyo ni moja ya visa vinavyosikitisha sana katika historia ya Tanganyika kwani aliwekwa kizuizini na Mwalimu Nyerere kama alivyofungwa na Waingereza. Haiwezekani kuwa Kawawa asiwe na habari na kile kilichopelekea mpigania uhuru hodari kama Ali Migeyo aishie jela tena wakati nchi ikiwa huru. Migeyo alifungwa na wakoloni kwa kuwahamasisha Watanganyika kudai uhuru labda Mzee Kawawa angeulizwa angeeleza ni nini kilitokea wakaamua kumfunga Migeyo kama walivyomfunga Waingereza.

Kitabu kimegusia kazi alofanya Kawawa kama mtumishi wa serikali ya kikoloni katika kambi za raia wa Kenyawalioshukukiwa kuwa ni Mau Mau.  Katika hawa wafungwa walikuwawepo wananchama wa TANU ingawa hawa walikuwa Wakenya. Maarufu katika hawa alikuwa Dome Okochi Budohi (ambae kadi yake ya TANU ilikuwa na 6) na Patrick Aoko. Budohi alicheza senema pamoja na Kawawa iliyoitwa “Wageni Wema.” Kawawa na Budohi walikuwa wakifahamiana vizuri sana kwa sababu wote walikuwa wasanii. Budohi alikuwa mmojawapo katika bendi ya vijana wa mjini iliyojulikana kama Skylarks. Bendi hii baadaye ilibadilisha jina na kuitwa Blackbirds. Matangazo ya radio yalipoanza Tanganyika, Blackbirds midundo ya Blackbirds ilikuwa haikosekani kusikika radioni katika Sauti ya Dar es Salaam. Kawawa kama walivyo vijama wote wa Dar es Salaam wa wakati ule alikuwa mmmoja wa wapenzi wa bendi hii na alikuwa hakosekani Ukumbi wa Arnatouglo bendi hii ikitumbuiza katika ile miaka ya 1950. Ilikuwa katika ule upigaji muziki wa Budohi ndipo alipoungana na Kawawa katika kutengenezwa kwa senama hiyo ya “Wageni Wema” ambayo mwandishi kaitaja lakini aliishia hapo tu.

Budohi na Aoko ni kati ya wafungwa wa Mau Mau waliokuwa Handeni ambako Kawawa alikuwa na jukumu la kuwaangalia. Budohi ndiyo alikuwa mtu wa kati baina ya TAA na KAU na kuanzia hali ya hatari ilipotangazwa Kenya mwaka 1952 Budohi na Aoko wakawa katika jicho kali la makachero. Makachero hawa Waafrika wanafahamika na wengine walikuja kufanya kazi hiyohiyo katika Tanganyikahuru.  Hiki ndicho kipindi ambacho Kaimu Rais wa TAA na Katibu wa TAA Abdulwahid Sykes alipokutana na Kenyatta Nairobi. Wakati Wakenya hawa wanafungwa Tanganyika, viongozi wa KAU akina Bildad Kaggia, Jomo Kenyatta, Kun’gu Karumba, Achieng Oneko, Paul Ngei na Fred Kubai walikuwa wamekamatwa Kenya. Kawawa ni mmoja kati ya viongozi hawa na ingependeza sana kama kupitia kwake tungeelezwa jinsi KAU na TAA ilivyokuwa ikishirikiana kwani haiwezekani kuwa Budohi na Kawawa uswahiba wao ukaishia kwenye kucheza senema tu.

Wanaharakati wote walishtushwa na kutiwa mbaroni kwa Budohi na Aoko. Haiwezekani kuwa iwe Mzee Kawawa kasahau matukio haya muhimu. Budohi na Aoko walikuwa wamefungwa minyororo walipokuwa katika selo pale Kituo cha Kati cha Polisi kwa sasa jumba hiloliko kituo cha mabasi kinachojulikana kama“station.”  Waliwekwa pale kwa miezi sita muda wote wakiwa na minyororo miguuni. Waliwekwa pale kwa miezi sita wakihojiwa kabla hawajapelekwa Handeni walipomkuta Kawawa. Hivi ndivyo vitu ambavyo kwa hakika vingeongeza ladha ya kitabu cha Mzee Kawawa endapo mwandishi angechukua muda kutafiti na kuzungumza na watu waliokuwa katika harakati wakati ule ambao bado wa hai kama Ally Sykes na mdogo wake Balozi Abbas Sykes na wengine wengi ambao walikuwepo wakati ule kama Mzee Chipaka.

Katika migomo ya wakati wa kudai uhuru hakuna mgomo uliofanikiwa na kuvuta hisia za wananchi kamamgomo wa reli wa mwaka 1960 uliodumu kwa siku 62. Ukiachia kutajwa tu kama sehemu ya historia undani wake na jinsi mipango yake ilivyokwenda na nafasi ya viongozi wa Tanganyika Railway African Union (TRAU) walivyopata misaada kutoka nchi za Mashariki hivi havijawekwa wazi. Si treni, meli wala mabasi ya railway yaliyotembea kwa mieizi mitatu. Mipango ya mgomo huu ilifanyika Tabora ambako ndiko palikuwa na karakana kuu ya reli na hapo ndipo palipokuwa makao makuu ya viongozi wa TRAU, Salum Abdallah mwenyekiti na Kassanga Tumbo katibu. Kawawa ana mengi katika kadhia hii kwa kuwa yeye wakati ule ndiye alikuwa Katibu Mkuu wa TFL. Inasemekana mgomo huu miezi michache kabla Tanganyika haijapata uhuru ndiyo ilikuwa kama zinduo kwa Mwalimu Nyerere kutambua kuwa hakuwa peke yake na sauti kwa wananchi. Walikuwapo viongozi wengine pembeni yake ambao nao wakipiga wananchi wanacheza. Ilimdhihirikia kuwa huko mbeleni wanakokwenda ipo siku atapambana na viongozi hawa. Hivyo ndivyo ilivyotokea.

Inasemekana Mwalimu Nyerere akimtumia Kawawa alianza mipango kabambe ya kujitayarisha hilolisitokee. Hii ilikuwa nukta muhimu sanakwani haukupita muda baada ya uhuru kupatikana mwaka wa 1961 viongozi hawa wa vyama vya wafanyakazi wakajikuta wamewekwa kizuizini. Wasomaji wangependa kujua Kawawa alijihisi vipi wakati viongozi wenzake wa vyama vya wafanyakazi aliofanya nao kazi wakati wa kudai uhuru wakishirikiana na TANU kama Victor Mkello, Paul Pamba, Abdallah Mwamba, Hassan Khupe, Salum Abdallah na wengine wengi walipokamatwa mwaka wa 1964 na kuwekwa kizuizini kwa amri ya Mwalimu Nyerere. Maelezo ya Mzee Kawawa katika mambo haya yangetia mwanga katika yale mengi yasiyofahamika katika historia ya Tanzania.

Waislam wangependa sanakujua hisia za Kawawa kama muumini alihisi vipi wakati makachero walipomvamia mzalendo aliyepigania uhuru wa Tanganyika Mufti wa TanganyikaSheikh Hassan bin Amir usiku wa manane na kumrudisha Zanzibar na kuwekewa masharti kuwa hana ruhusa kurejea Tanzania Bara. Nilitegemea kusoma sakata zima la kukamatwa kwa Sheikh Hassan bin Amir na kuvunjwa kwa East African Muslim Welfare Society (EAMWS) jumuia ya Waislam iliyokuwa ikipanga kujenga Chuo Kikuu Dar es Salaam.

Nilitegemea halikadhalika kusoma mchango wa Mzee Kawawa katika kuunda Bakwata. Mengi yamesemwa kuhusu hujuma hii kwa Waislam moja wapo ni kuwa EAMWS ilivunjwa kwa shinikizo la Kanisa Katoliki likimtumia Mwalimu Nyerere. Hili si jambo la siri tena tafiti mbalimbali zimefanywa na vitabu kuandikwa na waandishi kutoka nje ya Tanzania kuhusu tatizo hili la kujitokeza udini mapema baada ya uhuru kupatikana. Kwa kuwa Kawawa alikuwa pamoja na Mwalimu Nyerere na alishiriki katika kuunda Bakwata wananchi hasa Waislam wangenufaika kusoma hisia zake wakati maamuzi hayo yanapitishwa na serikali. Kwa hakika kuna maamuzi mengi sanaambayo Kawawa alishiriki yaliwaumiza sanaWaislam katika juhudi zao za kujitafutia elimu. Waislam wangependa sana kujua ni kipi kilikuwa kinamsukuma kufanya vile.

Kwa yeyote atakaepata bahati ya kusoma kitabu cha maisha ya Mzee Kawawa ni wazi hatakuta jipya ambalo hakuwa akilijua kabla. Kwa ajili hii basi mlango bado uko wazi kwa watafiti wengine kuandika kitabu kuhusu Rashidi Mfaume Kawawa kwani maisha ya Mzee Kawawa bado hayajaandikwa. Hata hivyo tumpongeze mwandishi kwa kazi hii kwani ni baada ya yeye kutuandikia kitabu ndipo nasi tumepata nguvu ya kunyanyua kalamu zetu na kusema.

3rd January 2010

Hapana Haja ya Kuiogopa Historia ya Uhuru wa Tanganyika

Mohamed Said

Mzee Yusuf Halimoja karudi tena safari hii anasema katika kichwa cha makala yake, “Sijasema Uhuru Uliletwa na Nyerere” (Jamhuri Januari 31 Februari 6 2012). Katika makala hii wakati mnakasha (majadilano)unanoga yeye katangaza kuwa anajitoa. Waswahili tuna msemo, “ametoa mbukwa.” Juu ya huko kujitoa madam kanitaja katika makala yake sina budi nami kumpa majibu yangu katika yale niyajuayo katika historia ya uhuru wa Tanganyika. Mzee Halimoja labda kwa utu uzima huwa anasema mengi. Mimi sitajibu kila aliloandika ila nitapita mle ambamo nahisi wasomaji watafaidika na kitu kipya ambacho hawakuwa wakikijua kabla ya hapo.

Si kweli kuwa Nyerere aliongoza juhudi za uhuru peke yake. Nyerere kaja Dar es Salaam mwaka 1952 na akapokelewa na rais wa TAA Abdulwahid Sykes na alikuta mambo yako mbali sana.  Kirilo kenda UNO  na kurudi, TAA ishazungumza na Kamati ya Umoja wa Mataifa inayosimamia nchi zilizokuwa chini ya Udhamini na ishapeleka mapendekezo ya katiba kwa Gavana Twining, TAA imeshaunda Kamati ya Siasa na ikapeleka viongozi wake (Abbas Sykes, Japhet Kirilo na Saadan Abdu Kandoro)  kutembea nchi nzima kuzungumza na wananchi kuhusu madhila ya  ukoloni. Juu ya hayo yote TAA imeshafanya uhusiano na  vyama vingine vya siasa kama African National Congress (ANC) ya Northern Rhodesia chini ya Kenneth Kaunda. (Ally Sykes hadi leo ana barua kadhaa alizokuwa akiandikiana na Kaunda kabla Kaunda hata hajauana na Nyerere). Vilevile Abdulwahid alikuwa kafanya mkutano na Kenyatta wakati wala Kenyatta hajasikia jina la Nyerere. Nia ya mikutano hii ilikuwa kuunganisha juhudi za TAA na KAU katika kupambana na Waingereza.

Kwa wengi mambo haya ni mageni katika masikio yao wameleweshwa na propaganda za TAA hakikuwa chama cha siasa. Simlaumu Mzee Halimoja naamini kabisa kuwa yeye haya hakuwa anayajua. Kwa Mzee Halimoja siasa Tanganyika haikuwezekana bila Nyerere na TANU chama ambacho Nyerere mwenyewe wala hana chimbuko nacho. Halimoja anazungumza kuhusu ujasiri wa Nyerere. Sawa hapana neno lakini je anaujua ujasiri wa Schneider Abdillahi Plantan katika TAA kiasi ambacho Waingereza walimkamata na kumweka kuzuizini? Je Halimoja anajua kisa cha Dome Okochi Budohi Mkenya kadi yake ya TANU na 6 kazi aliyokuwa akifanya katika harakati za TAA kabla hawajaunda TANU akiwa ndiye kiunganisho kati ya TAA na KAU ya Kenyatta? Ninaweza kumpa mifano kocho. Budohi alikamatwa mwaka 1955 pamoja na wanaharakati wengine wa Kenya kwa tuhuma za kuwa Mau Mau. Budohi alifungwa kisiwa cha Lamu kuazia 1955 hadi 1963 Kenya ilipokuwa inakaribia kupata uhuru ndipo alipoachiwa. Budohi akifahamiana vyema kabisa na wazee wangu na nimejifunza mengi kutoka kwake kuhusu TAA na TANU. Lakini kama Mzee Halimoja anataka kubaki na historia ya Nyerere inayoanza na TANU 1954 na kupuuza michango ya wengine mimi sina ugomvi na hilo. Naamini kwa haya machache msomaji kapata yale ambayo hakuwa anayajua kabla na keshatambua kuwa TAA kilikuwa chama cha siasa hata kabla Nyerere hajakutana na Abdu Sykes Dar es Salaam mwaka 1952.

Mzee Halimoja kazungumzia kuhusu Abdulwahid Sykes kuwa kwa nini natumia rejea zake. Napenda kumafahamisha kitu kimoja. Historia ya Nyerere na TANU itakuwa salama na ikafahamika kama inavyofahamika katika historia rasmi mfano wa hii ya Mzee Halimoja ikiwa tu Abdulwahid Sykes utamtoa katika historia ya TAA na TANU na historia ya Nyerere mwenyewe. Lakini pale tu utamkapomleta marehemu Abdu katika historia ya TAA na TANU itakubidi uachane na Nyerere kwanza na urudi robo karne nyuma kupata mwanzo wa harakati na hapo ndipo unapambana na Nyaraka za Sykes na hazitakuwa za Abdulwahid bali za baba yake. Hapo ndipo utakapojua umuhimu wa nyaraka hizi. Kueleza yaliyomo humo katika nyaraka hizo inataka mada itakayojitegemea yenyewe kwani ni historia inayorudi nyuma karne moja. John Iliffe aliondoka na baadhi ya nyaraka hizi ambazo alikabidhiwa na binti yake Abdu Sykes, Daisy Aisha wakati Daisy alipokuwa mwanafunzi wake wa historia miaka ya 1960 katikati Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na Iliffe hajazirejesha hadi leo. Nyaraka hizo ndizo zilizomsaidia Illife kuandika historia ya TAA. Kwa nini historia ya harakati ipatikane kwa mtu mmoja tu Abdu Sykes kama anavyouliza Mzee Halimoja, jibu lake ni hili, baba yake Abdu Kleist Sykes ndiye aliyeasisi harakati za siasa Tanganyika mwaka 1929 na ameacha nyuma hazina kubwa ya maandiko. Anaetaka kujua zaidi na asome “Kleist Sykes, The Townsman” na Daisy Sykes katika “Modern Tanzania,” kitabu kilichohaririwa na John Illife.

Mzee Halimoja anasema Nyerere ndiye aliyeandika katiba ya TANU. Nataka nimweke sawa Mzee Halimoja kuhusu katiba ya TANU. Katiba ya TANU haikuandikwa na yeyote yule. Kwa ufupi ni kuwa Nyerere hakuandika katiba ya TANU. TAA Political Sub Committee ilinakili katiba ya Convention Peoples Party (CPP) ya Kwame Nkrumah neno kwa neno. Mzee Halimoja akitaka ushahidi aitafute katiba ya CPP na aifananishe na katiba ya TANU. Hilo la kwanza. Kitu cha pili napenda kumsahihisha kwa heshima zote Mzee Halimoja kuwa hiyo ilani namba 14 aliyoeleza kuwa ilitolewa na Waingereza haikuwa namba 14 bali namba tano ikijulikana kama Government Circular No. 5 (1 August 1953) ikiwakumbusha viongozi wa TAA kutojiingiza katika siasa. Haya yalitokea baada ya serikali kuwa na ushahidi kuwa TAA ilikuwa inafanya siasa dhahir shahir jambo ambalo Mzee Halimoja hataki kulisikia sharti siasa iwe na Nyerere yumo. Baada ya kuona akina Abdu Sykes na Hamza Mwapachu hawasikii wameshikilia tu kuwasakama Waingereza na serikali yao ikatoka Government Circular No.6. Hapa kuna kisa cha kuhadithia lakini kwa makala hii tutajitoa nje ya maudhui. Kipindi hiki wengi walikikimbia chama wakabaki wanamji. Abdulwahid ilibaki kidogo apoteze kazi yake kama Market Master Soko la Kariakoo. Hii ndiyo historia ya siasa ya TAA na TANU niijuayo mie, historia ambayo wazee wangu walikuwa wachezaji wa kikosi cha kwanza na wakinihadithia siku zote hadi walipotangulia mbele ya haki. Jambo la tatu Mzee Halimoja hasemi kweli kuhusu historia ya TANU katika sehemu zile ambazo kanisa lilikuwa na nguvu. Ukweli ni kuwa waliochelewa kuingia TANU si Warufiji na Wangindo bali watu wa Masasi, Peramiho na kwengineko kutokana na shinikizo la Kanisa. Niruhusu msomaji mpenzi nikudokolee kidogo mambo kutoka katika hazina ya wazee wangu.

Mkutano wa kwanza wa TANU 1955 ulihudhuriwa na Salum Mpunga na Ali Ibrahim Mnjawale kutoka Lindi. Mkutano huu ulifanyika Dar es Salaam Ukumbi wa Hindu Mandal.  Baada ya mkutano, wakati wajumbe wengine wanaondoka kurudi kwenye majimbo yao, Mpunga na Mnjawale walibakia nyuma kukutana na uongozi wa makao makuu wa Julius Nyerere, Sheikh Suleiman Takadir, John Rupia, Ali Mwinyi Tambwe, Said Chamwenyewe, Oscar Kambona na wengineo. Mpunga na Mnjawale waliwafahamisha viongozi wa makao makuu kuhusu hali mbaya ya siasa Jimbo la Kusini. Mbali na kampeni za kuipinga TANU za Liwali Yustino Mponda ambae Mzee Halimoja anamfahamu vyema kabisa, katika ziara yake Lindi Gavana Twining aliwatahadharisha Waafriika wa Tanganyika wasijihusishe na “wafanya fujo” wanaotaka kuzusha vurugu. Twining alikuwa akitoa onyo hili akiikusudia TANU. Hotuba hii ya Gavana iliwatisha wananchi wengi kutoka sehemu za kusini kujiunga na TANU.

Mpunga na Mnjawale waliomba Nyerere aende majimbo ya kusini kuhamasisha wananchi ili wakabiliane na fitna za Gavana Twining na kampeni za kupinga TANU zilizokuwa zikiendeshwa na Liwali Yustino Mponda. Ukweli ni kuwa Nyerere hakutaka kwenda katika ziara ile akijua kuwa huko alikuwa anakwenda kupambana na kanisa lake uso kwa macho. Juu hayo yote Mpunga na Mnjawale katika kikao kile walimsisitizia Nyerere umuhimu wa yeye kwenda Lindi ambako kunaweza kuwa ndiyo chanzo cha TANU kupata ufanisi Newala, Songea, Tunduru na Masasi ambako kulikuwa na upinzani mkubwa dhidi ya TANU. Katika sehemu hizo Kanisa lilikuwa likiwazuia Wakristo kujiunga na TANU. Sheikh Suleiman Takadir, Said Chamwenye, John Rupia, Ali Mwinyi Tambwe wote waliunga mkono ule ujumbe wa Lindi juu ya suala hili. Baada ya kufikia makubaliano, Mpunga na Mnjawale walipewa barua ya kuthibitisha safari ya Nyerere. Ali Mwinyi Tambwe na Rajab Diwani walifuatana na Nyerere kwenda Jimbo la Kusini kuondoa wasiwasi na woga uliozushwa na Gavana Twining na kibaraka Yustino Mponda.

Nyerere na msafara wake ulipokelewa na uongozi wa TANU wa Lindi huko Mbanji, kijiji kidogo nje ya mji. Msafara wa Nyerere ulipowasili Mbanji ilikuwa kiasi cha saa moja jioni hivi na giza lilikuwa linaanza kutanda. Mbali na Mpunga na wale wajumbe wawili waliokutana na Nyerere mjini Dar es Salaam mwezi uliopita, hakuna hata mtu kati ya umma ule uliokuja kupokea ujumbe kutoka makao makuu ya TANU aliyekuwa anajua Nyerere anafanana vipi. Mpunga, dereva wa lori, alijibagua kutoka kwa lile kundi la watu akawa amesimama pembeni ili Nyerere apate kumuona. Baada ya Nyerere kumtia Mpunga machoni, Mpunga alimwendea kumsalimu Nyerere, Tambwe na Diwani; kisha aliligeukia lile kundi la watu kumtambulisha Nyerere kwa wananchi akilitaja jina lake kwa sauti kubwa. Baada ya hapo aliutambulisha ule ujumbe wa Nyerere. Nyerere na ujumbe wake ulisindikizwa kwa shangwe na kundi la watu hadi ofisi ya TANU kwenye nyumba ya Suleiman Masudi Mnonji. Kupakana na ofisi ya TANU ilikuwepo nyumba ya seremala mmoja, Issa bin Ali Naliwanda. Hii ndiyo nyumba iliyochaguliwa alale Nyerere na ujumbe wake, si kwa sababu ilikuwa nzuri kupita zote. Ilichaguliwa na kupewa heshima hii kwa sababu ilikuwa karibu sana na ofisi ya TANU na hivyo basi ilirahisishia TANU kazi ya ulinzi wa Nyerere. Siku iliyofuata ilikuwa Jumapili na Nyerere aliwaomba wenyeji wake apelekwe kanisani kwa ajili ya ibada.

Kanisa Katoliki mjini Lindi ni jengo la fahari lililoko ufukweni katika Bahari ya Hindi. Lindi ulikuwa mji wa Waislam. Mbali na mlio wa kengele za kanisa hakuna mtu pale mjini aliyekuwa akishughulishwa na kile kilichokuwa kikifanyika kwenye viwanja vya kanisa. Watu wachache waliokuwa wakienda kusali kanisani walikuwa Wakristo waliokuja Lindi kutoka sehemu nyingine za Tanganyika kufanya kazi katika ofisi za serikali. Ghafla mahala hapa palipokuwa pweke, palipopuuzwa kwa miaka na Waislam wa mjini, pakawa muhimu kwa sababu rais wa TANU ambae alikuwa Mkatoliki alikuwa na haja ya kuhudhuria ibada pale kanisani. Hakuna mtu katika uongozi wa TANU wa Lindi aliyejua ndani ya kanisa lile kulikuwa vipi wala hapakuwa na yoyote kati yao aliyewahi kuingia ndani ya kanisa, si Lindi wala mahali popote pale. Uongozi wa TANU wa Waislam mjini Lindi haukumwamini Mkristo yoyote kumsindikiza Nyerere kanisani ili kumpa ulinzi. Baada ya kujadili suala hilo kwa urefu hatimaye iliamuliwa kuwa Mpunga na wanachama wachache Waislam wenye kuaminika lazima wamsindikize Nyerere kanisani na wengine wabakie nje kulinda mlango.

Jumapili hiyo Nyerere aliingia ndani ya kanisa Katoliki mjini Lindi akifuatwa nyuma na walinzi wake Waislam wakiongozwa na Salum Mpunga, dereva wa lori shupavu. Misa hii maalum  ilidumu katika fikra za wale Wakristo waliokuwepo pale kanisani kwa miaka mingi kwa kuwa tukio hilo liliwagusa sana Wakristo walioshuhudia mkasa ule ndani ya kanisa la Lindi. Hii huenda ilikuwa mara ya kwanza na ya mwisho kwa Nyerere kumsalia Mungu wake huku akiwa amesimamiwa na Waislam. DC mkoloni alikataa kutoa kibali kwa TANU kufanya mkutano wa hadhara. Akiwa amekasirika sana, Shabaan Msangi aliitisha mkutano wa dharura wa tawi uliohudhuriwa na Nyerere na Tambwe. Baada ya mkutano huo Tambwe alikwenda kumwona DC. Ruhusa ilitolewa, na adhuhuri hiyo siku ya Jumapili, katika kiwanja ambacho Wazungu walikuwa wakicheza gofu, ambako mwaka mmoja uliopita Gavana Edward Francis Twining alitoa hotuba iliyowavunja moyo Waafrika, Nyerere alihutubia mkutano wa hadhara. Kamwe haijapata kutokea kabla ya siku ile katika historia nzima ya Jimbo la Kusini, watu wengi kiasi hicho kujumuika mahali pamoja. Wazungu na Wahindi pamoja na askari, watu wakiwa wamekaa na wengine wamesimama katika ya jua kali walikuja kumsikiliza Nyerere akihutubia. Ili kuhakikisha amani na usalama pale mkutanoni serikali iliweka askari waliouzunguka uwanja mzima wa mkutano. Nyerere aliwafikishia watu ule ujumbe wa TANU wa kuwa, kutawaliwa ni fedheha, na Waafrika wa Tanganyika lazima wadai uhuru wao. Uingereza ilikuwa ikiitawala Tanganyika chini ya udhamini kwa niaba ya Umoja wa Mataifa, na wakati ukiwa muafaka inabidi Uingereza ikabidhi nchi kwa wananchi wenyewe. TANU ilikuwa imewasili Jimbo la Kusini.

Wasomaji wapenzi katika makala yangu iliyopita nilimpa changamoto Mzee Halimoja aeleze ni akina nani waliingiza TANU kwao huko Masasi na Peramiho. Ukweli ni kuwa hata kugusia hili katika makala yake iliyopita hakuthubutu. Nimempa changamoto aeleze hicho anachokiita “mchango wa pekee wa Nyerere” katika kupigania uhuru wa Tanganyika. Hilo vilevile limemshinda. Nashukuru kuwa kanijibu ingawa kakwepa baadhi ya mambo muhimu lakini kwa kufanya hivyo kanipa mimi nafasi ya kueleza yale ambayo naamini wengi walikuwa hawayajui. Nyerere hakuwa peke yake katika kuupigania uhuru wa Tanganyika wala hakuandika katiba ya TANU wala harakati za kupigania uhuru hakuzianzisha yeye. Nadhani haya niliyoandika yanatosha kwa sasa na ningependa kumaliza kwa kuuliza swali. Nani leo anawakumbuka wazalendo hawa nilowataja katika makala haya? Je hawastahili watu hawa kuenziwa pamoja na Nyerere?


30 Januari 2012

Muslims and the Negative Press: Bakwata Once Kibaraka Always Kibaraka The Case of the Late Prof. Kigoma Ali Malima

Muslims and the Negative Press: Bakwata Once Kibaraka Always Kibaraka
The Case of the Late Prof. Kigoma Ali Malima

By Mohamed Said

...after his resignation from the CCM many Muslims went to see Prof. Malima to congratulate him. The political committee went to congratulate him for his resignation from the government as Minister of Trade and Industries. Then two days later Prof. Malima through Sheikh Khalifa Hamis suddenly summoned the committee to his constituency in Kisarawe where a meeting was held. After salat isha Prof. Malima told the committee that he has accepted their proposal and NRA should start preparations for meeting of the National Conference to be held in Tabora from where in a public rally he would announce his resignation from the CCM. At that time NRA had managed to establish branches in Kigoma, Mpwapwa, Igunga and Tabora.

Sheikh Khalifa Hamis went to Tabora to prepare the terrain for Prof. Malima’s trip to the town. NRA had a branch in Tabora but it had scanty membership. The chairman of NRA Tabora branch was a retired army captain Mustapha Kivuruga, son of Abdallah Kivuruga founder member of the TAA in Tabora in 1945 and founder member of TANU in 1955. Mustapha Kivuruga joined the army and was trained in Israel. Abdallah Kivuruga and his brother Maulidi Kivuruga had been important personalities in the local politics of Tabora. Sheikh Khalifa held a meeting with the cream of the Muslim activists in Tabora at the Nujum Muslim Centre.  Among those in attendance was Bilal Rehani Waikela [1] a veteran of the Muslim struggle against injustices and Christian hegemony.

The activists were informed that Prof. Malima was coming to Tabora and would announce his resignation from CCM at a public rally. It was now upon them to lay down strategy for the success of Prof. Malima’s trip and revitalisation of NRA. Following this meeting elections were called at the Adult Education Centre and Waikela was elected NRA Tabora Regional Chairman replacing Kivuruga. Kivuruga became district chairman. It was from this meeting that membership drive for the NRA began. Tabora has always carried with it a grudge against the government. The place was completely forgotten. Like many Muslim areas, no meaningful development had taken place since independence. The people in Tabora saw this as there opportunity to have their own back against the government and the CCM.

Prof. Malima and his entourage were booked to fly to Tabora on Friday morning aboard Air Tanzania. Their bookings were confirmed but when they presented their tickets, they were told that the flight was fully booked. Their protests to the fact that there bookings were confirmed fell into deaf ears. Prof. Malima decided to travel to Tabora by road.[2]Meanwhile the Christian Lobby had been busy. It had constantly working on plots to discredit Prof. Malima in the eyes of the right thinking people. The press both private and that owned by the government and party, including the state-owned radio; and the office of the president, has been Muslim’s worst enemy in its struggle against injustice. The media fabricates and publishes negative stories about Muslims with impunity.

The propaganda is given an angle of Muslim radicals harbouring the desiring to overthrow a legally constituted government. Muslims have suffered in this campaign with Prof. Malima. The Friday papers Majira, Nipashe, including CCM daily Uhuru and the Tanzania News Agency (SHIHATA)  carried stories in banner headlines that Prof. Malima was on that day Friday the 15 July, 1995 going to announce his resignation from CCM at Tabora in the Friday Mosque after Friday Prayers. What this negative publicity wanted to achieve was to portray Prof. Malima as dangerous man who wanted to pit Muslims against Christians to acquire power for his own selfish ends. The end result for such an eventuality was obvious civil upheavals.

On that Friday morning Muslim notables and leaders and members of the NRA in Tabora went to the Air Port to meet Prof. Malima. The plane flew in without him. In Tabora town rumor was spreading that Pro. Malima was to address Muslims and announce his resignation from CCM from the pulpit of the Tabora Friday Mosque. Even before the time for the Friday prayers was due, the Friday Mosque was filled to capacity and some of the worshippers were sitting sprawled outside the mosque grounds. But few knew that Prof. Malima was not in Tabora that day anyway. The previous day Regional Police Commander called on the BAKWATA leadership in Tabora and informed them that Prof. Malima was to address Muslims at the Friday Mosque. The police commander insisted upon BAKWATA leadership that that was mixing religion and politics; and that was not acceptable. The government would not allow house of worship to be used as political arena.  It was therefore up to BAKWATA to ensure that Prof. Malima does is not allowed to announce his resignation from the CCM from the pulpit. Security personnel were deployed to the mosque early morning on Friday. There were uniformed and plainclothes policemen on beat around the Friday Mosque since day break.  In the afternoon police cars arrived at took strategic positions around the mosque. State Intelligence personnel were very much in evident mingling with Muslims outside the mosque. This created tension inside and outside the mosque.

Few minutes before prayers were to begin; Sheikh Mavumbi from BAKWATA arrived at the mosque in a police car escorted by the Regional Police Commander. Sheikh Mavumbi went infront of the mosque and through the public addressing system he warned of the dangers of mixing religion and politics. People were dead silence listening to Sheikh Mavumbi. He said he has been informed that Prof. Malima was to address Muslims from the mosque that day and he has come to announce that he is forbidden to do that in that mosque. As soon as he uttered Prof. Malima’s name there was pandemonium in the mosque, Muslims shouting asking Sheikh Mavumbi his source of that information. Sheikh Mavumbi seemed confused as there were shouts from every angle of the mosque. Muslims looked threatening and the mood inside the mosque was fiery.  Tabora Friday Mosque is under Imam Issa Mzee, a young man in his mid-thirties. He rose up to calm Muslims but people were not listening to him. 

As things seemed to get out of control and other Muslims were rising standing up from where they had been sitting and the crowd outside the mosque was fighting to get inside the mosque, there was indication that the sanctity of that holy place was going to be violated. It was then that Waikela moved to the front of the mosque and took up the microphone and called for peace. Seeing Waikela at the kibla calm prevailed and Waikela told Muslims not to blame Sheikh Mavumbi for his announcement. It was probable he had been told to come to the mosque to make the announcement. The best way for Muslims to do was not to condemn Sheikh Mavumbi but to ask him who told him that Prof. Malima would come to the mosque to deliver a political address. Appealing to Muslims Sheikh Waikela asked them if anyone had seen Prof. Malima in the mosque. The crowd answered in the negative.

Islamic law demands that when there is a controversy between two parties, both parties should be heard before passing judgement. Sheikh Mavumbi had judged Muslims without giving them chance to be heard. Amidst boos from Muslims, Sheikh Mavumbi ashamed was led out of the mosque through the back door of the mosque and on into the waiting police car. Was he to walk out from the main door Muslims would have beaten him. It was then when the police were whisking him away from his fellow Muslims that Sheikh Mavumbi realised that he had been a fool and the government had used his religious position among Muslims for its own political ends. People have simple minds. Any announcement through the radio or the printed word is bound to be taken as the truth. For how could the government allow its media to be used for propaganda and spread lies against Muslims?  If an announcement is on the radio and newspapers then it is the truth. Sheikh Mavumbi like many people in Tabora believed in what they read and heard on the radio that Prof. Malima was going to make a major political statement from the pulpit. On that Friday Prof. Malima spent the night in Nzega and arrived in Tabora Saturday afternoon and stayed at the house of Suleiman Marjebi one of the notables of  the township.

On Sunday 17 July, 1995 thirty-seven years since TANU held its 1958 annual meeting in Tabora the meeting which paved the way to independence, Prof. Malima addressed a big rally at Uyui grounds. The Tabora meeting would be remembered for its achievement. It managed to put into Legislative Assembly Julius Nyerere, Chief Abdallah Said Fundikira, John Ketto, Nesmo Eliufoo, John Mwakangale, Lawi Sijaona and Paul Bomani. It was in Tabora that Nyerere shed tears because of oppression of which Tanganyikans were being subjected to by the British. Nyerere said if the British did not want to set Tanganyikans free he would direct his anguish to God. Before Prof. Malima spoke Bilal Waikela mounted the platform dressed in his prison uniform which he wore thirty years ago when he was detained by Nyerere for resisting Christian hegemony. He reminded the people of Tabora that he was detained by Nyerere for reminding him of the cherished ideals of TANU the party they had formed and built together in order for Africans of Tanganyika to be free from all forms of oppression. Waikela told his audience that and he was now returning to politics to seek for that equality and justice denied.

Prof. Malima announced his resignation from the CCM at the Uyui meeting. Prof. Malima told his audience that that oppression which made Nyerere shed tears while giving a speech to members of TANU and the people cried with him at the Tabora Central Market was still prevalent 37 year after the tears had long dried. Prof. Malima told his audience that he was resigning from the CCM because, he said, the party has deviated from its cherished ideals of justice and equality and had established classes. He was resigning and joining the opposition in order to fight for equality among all the people in Tanzania.

That Sunday night NRA National Conference was held and Prof. Malima was elected Chairman and Abubakar Olotu secretary of NRA. What had taken place in Dar es Salaam Airport repeated itself in Tabora Railway Station. NRA had booked a wagon for its delegates travelling back to Dar es Salaam and had paid for it in advance. But when they arrived at the railway station, they were told that no wagon has been allocated to them. The press had the chance to correct their earlier story that Prof. Malima had planned to announce his resignation from the mosque but it did not do so. The propaganda machinery wanted people to believe that Prof. Malima was unable to do so because Muslims did not allow him to mix “religion and politics.”



Sheikh Bilal Rehani Waikela TANU founder member Tabora, 1955 and secretary of  East African Muslim Welfare Society (EAMWS), Western Province. Picture taken at Kisutu Resident Magstrate Court with Advocate Juma Nassoro.


[1] For more information on Bilal Rehani Waikela see Mohamed Said, "Islam and Politics in Tanzania," Al Haq International, Karachi, Vol. 1/No.3, August- December, 1993.
[2] Majira,15 July, 1995.

Unadhani kuwa nani anasifa ya kuwa rais wa Tanzania?