Home » , » SHEIKH CHAMBUSO RAJAB RAMADHANI CHAMBUSO

SHEIKH CHAMBUSO RAJAB RAMADHANI CHAMBUSO

Written By mahamoud on Thursday, 26 December 2013 | 20:43




Sheikh Chambuso akigawa mashaf kwa wanafunzi wake katika shule ya St. Christine Tanga anaowasomesha somo la Islamic Knowledge. 

Sheikh Chambuso mbali na kusomesha Uislam katika shule za sekondari vilevile yeye ni mmoja wa walimu katika mojawapo ya shule ya awali aloaanzisha pamoja na vijana wenzake Mabawa Tanga. Sheikh Chambuso pia ni Imam katika moja ya misikiti maarufu ya Tanga.

Mbali na kusomesha Qur'an Sheikh Chambuso ni mlezi wa vijana na mshauri katika masuala ya elimu na tabia njema kwa vijana wetu.

Ilikuwa katika moja ya kazi zake kuwatumikia Waislam ndipo alipokamatwa Tanga mjini akawekwa rumande, akatishwa na mwishowe alipelekwa Handeni kulipotokea mauaji ya Waislam Oktoba na huko akafunguliwa mashtaka ya kubambikizwa ya ''kushawishi mauaji.''

Sheikh Chambuso alikaa mahabusu kwa takriban wiki mbili na ilikuwa katika kipindi hicho alipokuwa mahabusu ndipo allipoelezwa dhulma walizofanyiwa Waislam wa vijiji vya Madina, Dibungo na Lwande.

Hii ikamfanya Sheikh Chambusio kuwa mtu wa kwanza kutoka Tanga kuwa na taarifa kamili ya kile kilichotokea katika vijiji hivyo.

Sheikh Chambuso anasema alifarajika sana siku ndugu zake walipofika rumande pale Handeni wakamletea gazeti la Annur ambalo ukurasa wa mbele ilichapwa picha yake na taarifa ya kukamatwa kwake.

Sheikh Chambuso anasema siku hiyo gazeti la Annur lilikuwa kivutio kikubwa kwa askari na kila askari aliliomba nagalau na yeye apitie asome habari za Sheikh Chambuso na kukamatwa kwake Tanga.

Hivi sasa yuko nje kwa dhamana. 

Sheikh Chambuso anasema kwa kupata mtihani huu yeye amefarajika sana kwani katika mihangaiko hiyo mpaka ndani ya jela amekutana na baadhi ya vijana ambao yeye aliwasomesha dini katika shule mbalimbali za Tanga na wengine akiwasalisha katika msikiti wake.

Sheikh Chambuso anasema kote huko wanafunzi wake aliowakuta ndani ya kazi zao walikuwa wakiinamisha viichwa vyao mbele yake na kuwekea heshima ya hali ya juu.

In Sha Allah tutakuwa wazi hapa kwa kipindi chote cha kesi ya Sheikh Chambuso na tutaweka taarifa zote zake yeye na za ndugu zetu wa Madina, Dibungo na Lwande.

Itaaendelea...In Sha Allah....




Share this article :

Post a Comment

Unadhani kuwa nani anasifa ya kuwa rais wa Tanzania?