Wakati mamilioni ya watu duniani kote walikuwa
wakifuatilia na kuvutiwa na hotuba zilizokuwa zikitolewa katika
shughuli ya mazishi ya mzee Nelson Mandela, jumuiya ya kimataifa
ya watu wenye ulemavu wa kusikia imeelezea kughadhibishwa kwake na kile
walichosema kuwa mkalimali wa lugha ya alama aliyetumika katika
shughuli hiyo alikuwa mkalimani bandia.
Kwa mujibu wa ripoti
iliochapishwa kwenye mtandao wa SBS News wa Australia, mlemavu kutoka
Afrika Kusini na ambaye ni mwanachama wa Tawi la Vijana la Shirikisho la
viziwi duniani, Braam Jordaan, alisema kuwa mkalimani huyo alikuwa
akijitengenezea alama zake mwenyewe ambazo hazipo kabisa kwenye lugha ya
alama.
Jordaan anadai kuwa ishara za mikono, uso na harakati
za mwili hazikuwa zikifuata kile kilichokuwa kikisemwa na mzungumzaje,
na kwamba tukio hilo limetia aibu katika shughuli hiyo muhimu kwa taifa
lake.
Mwakilizi wa Jumuiya ya Wakalimani wa Lugha ya Alama
ulimwenguni, Sheena Walters naye pia aliuambia mtandao wa SBS kuwa
harakati za mikono zilizokuwa zikitumiwa na mkalimani hazitambuliki
katika aina yoyote ya lugha ya alama.
Sheena alisema kuwa lugha
nyingi za alama duniani zina muundo na mfumo unaofanana na kwamba
mkalimani huyo alikuwa akirudiarudia alama zilizoonekana kutofahamika au
kuonekana kwa wanaomfuatili.
Wakati shughuli za mazishi
zikitangazwa moja kwa moja na vyombo vingi vya habari ulimwenguni,
wanachama wa jumuiya hiyo ya viziwi walimiminika kwenye mtandao wa
kijamii wa Twitter kuelezea hasira zao juu ya tukio hilo.
Kwa
mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, chama tawala cha Afrika ya
Kusini, ANC kimekuwa kikimtumia mkalimani huyo, na kiliwahi kulalamikiwa
juu ya udhaifu wake.
(Pichani: Mkalimani wa Lugha ya Alama akiwa pembezoni mwa Rais Obama)
MKALIMANI WA LUGHA YA ALAMA KWENYE MSIBA WA MANDELA AZUSHA KIZAAZAA
Written By mahamoud on Saturday, 14 December 2013 | 06:42
Labels:
adverts
Post a Comment