Home » » JINSI YA KUPIKA ROAST LA KUKU

JINSI YA KUPIKA ROAST LA KUKU

Written By mahamoud on Saturday, 14 December 2013 | 06:33


MAHITAJI

Kuku mmoja 1
Vitunguu maji 3
Vitunguu swaumu 1
Unga wa binzari paketi 1
Unga wa pilipipili mwekundu paketi 1 1/2
Pilipili manga paketi 1
Mafuta ya kupikia robo 1/4
Girigilani
Tangaizi
Nyanya maji
Maggi
Ndimu

JINSI YA KUANDAA

1:Chemsha kuku wako pamoja na tangawizi,kitunguu swaumu, unga wa binzari,pilipili manga,chumvi na ndimu ili kuweka ladha nzuri,

Muache kuku wako aive
Akisha iva mtoe katika supu na umuweke pembeni.

2:Chukua sufuria nyingine tia mafuta yakichemka kaanga kuku wako hadi awe rangi ya kahawia au brown

3:kisha mtoe kuku wako katika mafuta,ili utumie mafuta hayo kwa kuweka vitunguu na ukaange kwa dakika 7-10kisha weka unga wa binzali,unga wa pilipili mwekundu,unga wa girigilani,mbegu za hiliki na nusu ya mbegu za pilipili manga.

4:Changanya vizuri hadi upate mchanganyiko mzuri mkavu,miminia humo ile supu uliyo iacha hapo awali

Wekapembeni ipowe .kisha kaanga nyanya zako ambazo ni fresh.katika sufuria nyingine .naupike hadi maji yaishe naibakie kama mafuta yakielea.kwa juu.

5:kisha mimi sosi yako katika kuku,na punguza moto acha achemke ili viungo vichanganyike na kuleta ladha nzuri utakapo ona mchuzi uneisha nakubaki rost unaweza epua na kuweka pembeni.

Nahapo kuku wako atakuwa tayari kwakuliwa na chochote utakacho.
Share this article :

Post a Comment

Unadhani kuwa nani anasifa ya kuwa rais wa Tanzania?